Umoja wa Mataifa unaendelea kutoa misaada kwa Niger, wiki tatu kufuatia Rais Mohamed Bazoum kushikiliwa na walinzi wake.
Msemaji wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric amesema mashirika ya umoja huo yanaendelea kuwafikia watu wenye mahitaji licha ya changamoto zilizopo, ikiwemo msimu wa sasa wa mvua.
Kwa mujibu wa msemaji huyo, watu milioni 4.3 nchini Niger wanahitaji msaada wa kibinadamu.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres, pamoja na wawakilishi wengine waandamizi wa umoja huo, wameendelea kutoa wito wa kuachiliwa kwa kiongozi huyo aliyechaguliwa kwa njia ya kidemokrasia, ambaye kwa sasa anazuiliwa nyumbani.