Kamati ya haki za binadamu ya Ethiopia EHRC inayoungwa mkono na serikali imeeleza wasiwasi juu ya athari ya haki za binadamu inayoletwa na mapigano ya kisilaha dhidi ya raia wa kawaida katika jimbo la Amhara.
Wito huu wa dharura umetolewa kufuatia mapigano ya siku kadhaa kati ya jeshi la serikali na wapiganaji wa huko wanaojulikana kama Fano katika jimbo la Amhara, jimbo la pili kwa idadi kubwa ya watu nchini Ethiopia.
Wito wa Kamati ya EHRC pia unatokana na shambulizi kali lililoripotiwa kusababisha vifo vya watu zaidi ya 26 katika mji wa Finote Selam, umbali wa kilomita 385 kutoka Addis Ababa.