Kampuni kubwa ya teknolojia ya China Huawei kuongeza uwekezaji jijini Dar
2023-08-15 14:00:42| cri

Kampuni kubwa ya teknolojia ya China, Huawei imeahidi kuimarisha uwekezaji wake nchini Tanzania baada ya kampuni hiyo kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha wa Tanzania Dk. Mwigulu Nchemba.

Hivi karibuni Huawei ilisaini dola za Marekani milioni 15.9 (takriban shs bilioni 37.3/-) na Kampuni ya Mawasiliano Tanzania (TTCL) kwa ajili ya kupanua Mkonga wa Taifa wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (NICTBB) hadi wilaya 23.

Mwaka huu, mapato ya kampuni ya Huawei yaliongezeka kwa asilimia 3 katika nusu ya kwanza. Taarifa kutoka Wizara ya Fedha ilisema Makamu wa Rais wa Huawei, Zhang, alimkaribisha Dk Nchemba na ujumbe wake ambapo wawili hao walijadili zaidi uwekezaji wa Kampuni hiyo nchini Tanzania.

Dkt.Nchemba aliambatana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Balozi wa Tanzania nchini China, Balozi Mbelwa Kairuki, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Bw. Masanja Kadogosa, Mkurugenzi Mtendaji wa TANROADS, Mhandisi Mohamed Besta miongoni mwa wajumbe wengine.