Mwanamume aliye na ‘familia kubwa zaidi duniani’, azikwa katika shughuli ya nadra kuonekana
2023-08-15 14:01:15| cri

Shughuli ya nadra kuonekana ya maziko ilifanyika Jumapili katika kijiji cha Naisinyai, Wilaya ya Simanjiro, Mkoa wa Manyara ambapo ndugu, wanakijiji na viongozi wa kisiasa walihudhuria kumzika mzee wa miaka 93 ambaye anaweza kuwa na jina la mtu mwenye familia kubwa zaidi duniani.

Maliake Laizer, ambaye alikuwa na jumla ya wake watano, ameacha jumla ya wanafamilia 307 wakiwemo watoto 41, wajukuu 219, vitukuu 45 na vinying’inya wawili. Mkuu wa Wilaya Dk.Suleiman Serere aliongoza mamia ya waombolezaji waliojitokeza kumsindikiza Mzee Laizer.

Kwa mujibu wa familia, Laizer alifariki dunia muda mfupi baada ya kukimbizwa katika zahanati baada ya kujisikia vibaya. Na mara moja ikaandaa mlo wa familia. Mwanawe, Mchungaji Joshua Maliake alisema baba yake alikuwa na wake wanne lakini alioa tena mke wa tano baada ya kufiwa na mmoja wa wake zake ili kudumisha idadi hiyo kufikia wanne.