UM: Mgogoro wa Sudan umesababisha majanga makubwa ya kibinadamu
2023-08-16 08:40:05| CRI

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yameonya kuwa mgogoro wa Sudan uliodumu kwa miezi minne sasa umesababisha majanga makubwa ya kibinadamu na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Msemaji wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR William Spindler, amewaambia wanahabari kuwa tangu mgogoro wa Sudan uibuke mwezi Aprili, watu zaidi ya milioni 4.3 wamelazimika kukimbia makwao.

Msemaji wa Shirika la Afya Duniani WHO Margaret Harris amesema mgogoro huo umeathiri vibaya maisha, afya na maslahi ya watu wa Sudan, ambapo asilimia 63 ya hospitali nchini humo zimesitisha huduma kwenye maeneo yaliyoathirika.

Msemaji wa Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa (OHCHR), Elizabeth Throssell amesema takwimu zisizo kamili zinaonesha kuwa zaidi ya watu elfu nne wameuawa, wakiwemo mamia ya raia wa kawaida.