Tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia yatoa mafunzo kwa makamanda 26 wa polisi ili kuinua hali ya usalama
2023-08-16 08:53:26| CRI

Tume ya mpito ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS) imesema imekamilisha mafunzo ya siku 10 kwa makamanda 26 wa Jeshi la Polisi la Somalia (SPF) ili kuongeza ujuzi wao wa kukabiliana na uhalifu na kusaidia kuimarisha usalama. 

Tume hiyo imesema mafunzo ya kina ya kinadharia na kiutendaji kuhusu usimamizi wa vituo vya polisi, yaliyofanyika mjini Mogadishu. Naibu Kamishna wa Polisi wa tume hiyo Bwana Martin Amoru, amesema katika taarifa iliyotolewa mjini Mogadishu kuwa makamanda wa polisi ni kiini cha usalama wa jamii, na sehemu muhimu ya juhudi zinazoendelea za kuleta utulivu nchini Somalia.

Mafunzo hayo yalihusu mbinu za kuchunguza uhalifu, kukamata, kuweka kizuizini, kupekua na kukamata, na mafunzo mengine muhimu.