Tanzania yazuia lori la mafuta lililokuwa linasafirisha wahamiaji haramu 65 wa Ethiopia
2023-08-16 09:13:52| CRI

Mamlaka za Tanzania zimesema kuwa zimezuia lori moja la kubebea mafuta lililokuwa linasafirisha wahamiaji haramu 65 wa Ethiopia kusini mwa nchi hiyo.

Mkuu wa wilaya ya Mlele mkoani Katavi Bw. Majid Mwanga, amesema gari hilo lilikuwa linalotoka mkoani Mwanza kuelekea Zambia, na lilizuiliwa saa saba mchana na maofisa wa uhamiaji na mawakala wa Huduma za Misitu baada ya kugundua kuwa kifuniko cha tanki la lori hilo kuwa wazi na kuwaona wahamiaji hao haramu.

Baada ya kuthibitisha hali zao za afya, walikabidhiwa kwa mamlaka za uhamiaji kwa ajili ya taratibu nyingine za kisheria.