Tanzania kuwa mwenyeji wa Kongamano la 13 la AGRF mwezi Septemba
2023-08-16 11:06:56| cri

Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Kongamano la 13 la Mifumo ya Chakula Afrika la kila Mwaka (AGRF) linalotarajiwa kuanza Septemba 5 hadi 9 mwaka huu katika Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe ameyasema hayo mjini Dodoma akibainisha kuwa zaidi ya washiriki 3,000 wanatarajiwa kuwepo katika kongamano hilo wakiwemo wadau wa sekta ya kilimo duniani, wawekezaji wa maendeleo, taasisi za fedha, watafiti, wafanyabiashara wa kilimo, wakulima wakubwa na viongozi wa serikali.

Alisema Tanzania ilipata fursa ya kuwa mwenyeji wa kongamano hilo baada ya kufanikiwa kushiriki katika shindano la kuandaa tukio kubwa la kilimo barani Afrika, (AGRF).