Nakisi ya bajeti ya matumizi ya Kenya kwa mwaka 2023 imepungua
2023-08-16 08:52:47| CRI

Nakisi kwenye bajeti ya matumizi ya Kenya hadi kufikia Juni 2023 imetajwa kupungua hadi shilingi za Kenya bilioni 666 (dola bilioni 4.63 za Marekani), ikilinganishwa na dola bilioni 5.833 za mwezi Juni 2022.

Kwa mujibu wa taarifa ya robo mwaka ya mapitio ya uchumi iliyotolewa na hazina ya Kenya kwa robo ya nne ya mwaka wa fedha 2022/2023, kupungua huko kumetokana na kuboreshwa kwa uwiano wa manunuzi na mapato.

Hazina ya Kenya imesema akiba ya manunuzi imeboreshwa kwa dola za kimarekani bilioni 1.3, hasa kutokana na kuboreshwa kwa mapato ya mauzo ya nje na kupungua kwa uagizaji bidhaa.

Ripoti pia imesema katika kipindi hicho mauzo ya nje yaliongezeka kwa asilimia 2.1 kutokana na ongezeko la uuzaji nje wa chai na bidhaa za viwandani.