Bunge la Kenya lata ripoti kuhusu kontena 49 za sukari iliyotakiwa kuharibiwa
2023-08-16 09:14:54| cri

Bunge la Kenya limeitisha ripoti ya mashirika mbalimbali kuhusu kontena 49 za sukari ambayo imechukua muda mrefu kuharibiwa.

Kamati ya Bunge la Kenya kuhusu Biashara, Viwanda na Ushirika ilibaini kuwa, kontena kadha zilizotakiwa kuharibiwa Mombasa bado zimehifadhiwa kwa zaidi ya miezi 19 sasa.

Wabunge hao waliomba ripoti ipelekwe kwa Kamati kwa muda wa siku 14, ili kueleza kwa nini hadi sasa kontena hizo bado ziko kwenye Kituo cha Mizigo cha Focus (CFS) katika Bandari ya Kenya (KPA).

Wabunge hao walielezea hofu ya kuendelea kuhifadhi sukari hizo mbovu kufuatia kisa cha miezi michache iliyopita, ambapo sukari nyingine iliyonuiwa kubadilishwa kuwa ethanol ilitoweka na kuhofiwa kuingizwa sokoni.