Wakuu wa kijeshi wa Afrika Magharibi kujadili mzozo wa Niger wiki hii
2023-08-16 11:07:37| cri

Wakuu wa kijeshi kutoka Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (Ecowas) watakutana nchini Ghana wiki hii kujadili uwezekano wa kuingilia kati mzozo wa Niger.

Mkutano huo wa Alhamisi na Ijumaa, ambao awali ulipangwa kufanyika wikendi iliyopita lakini ukaahirishwa, unafanyika baada ya viongozi wa Ecowas wiki iliyopita kuidhinisha kutumwa kwa "kikosi cha kusubiri ili kurejesha utulivu wa kikatiba" nchini Niger, ambayo rais wake alipinduliwa Julai 26.

Mkutano wao wa kilele uliofanyika katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja Alhamisi iliyopita, pia ulithibitisha matakwa ya jumuiya ya kupata matokeo ya kidiplomasia.