Kenya yaongoza kwa watu wanaomiliki simu za mkononi
2023-08-16 09:15:21| cri

Asilimia ya watu wanaom,iliki siku za mkononi nchini Kenya imeongezeka hadi 64 kutoka 61 mwaka wa 2021, silimia 64 mwaka jana ikilinganishwa na asilimia 61 mwaka wa 2021, hali inayoashiria ongezeko la upatikanaji wa wateja kwa kampuni za mawasiliano za Safaricom na Airtel Kenya.

Idadi hiyo ya watu wanaomiliki simu za mkononi nchini Kenya ndio wa juu zaidi katika kanda, mbele ya Zambia (asilimia 57 mwaka 2022), Tanzania (asilimia 54), Nigeria (asilimia 48), Uganda (asilimia 45) na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (asilimia 44). Mamlaka ya mawasiliano nchini Kenya CAK imesema watumiaji wengi wanalamizika kutumia laini zaidi ya moja za simu ili kufaidika na ofa mbali mbali zinazotolewa na kampuni za mawasiliano.