Idadi ya wageni waliotembelea Namibia mwaka 2022 yaongezeka kwa asilimia 98.1
2023-08-16 09:18:34| CRI

Ripoti iliyotolewa jana ya takwimu za watalii waliowasili nchini Namibia kwa mwaka 2022, inaonesha kuwa idadi ya watalii wa kimataifa walioingia nchini Namibia imeongezeka kwa asilimia 98.1, kutoka laki 2.3 wa mwaka 2021 hadi laki 4.6 wa mwaka jana.

Waziri wa mazingira, misitu, na utalii wa Namibia Bw. Pohamba Shifeta, amesema takwimu za idadi ya watalii ya mwaka 2022 zinaonesha kufufuka kwa asilimia 28.9. Kutokana na ufufuaji wa kasi wa sekta hii, wizara hiyo inawahimiza wasimamizi wa maeneo, waendeshaji wa shughuli za watalii, na wadau wote kuandaa mipango mipya, njia mpya, na maeneo mapya ya kutalii, hatua ambayo itaongeza uzoefu wa wageni na kuvutia wageni watakaokuja tena.