Afrika yanufaika na uhusiano wa biashara na uwekezaji na China
2023-08-17 09:10:56| CRI

Katibu mkuu wa Shirika la Biashara na Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNCTAD) Rebeca Grynspan, amesema Afrika inanufaika na uhusiano wa biashara na uwekezaji kati yake na China.

Bibi Grynspan ameyasema hayo mjini Nairobi kwenye mkutano wa shirika hilo wa kutoa ripoti ya mwaka 2023 kuhusu maendeleo ya uchumi barani Afrika.

Amesema China ni nchi muhimu inayowajibika, na imeibuka kuwa mshirika muhimu wa kibiashara kwa nchi za Afrika pamoja na nchi nyingine za Kusini, wakati inapata maendeleo ya uchumi katika miongo kadhaa iliyopita.

Amebainisha kuwa China inaweza kuzisaidia nchi za Afrika kuimarisha biashara ya kimataifa, kwa kuwa ina teknolojia na minyororo muhimu ya ugavi. Aidha, China pia inaweza kuzisaidia nchi hizo kuongeza thamani ya malighafi zake.