EAC yapanga kuandaa mkutano wa kilele wa biashara kati ya Afrika, China na Marekani
2023-08-17 10:50:31| cri

Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) inapanga kuandaa Mkutano wa kilele wa Biashara kati ya Afrika, China na Marekani wa mwaka 2024.

Hayo yamezungumzwa katika mkutano kati ya Katibu Mkuu wa EAC, Dk Peter Mathuki na Rais wa Jumuiya ya Wakurugenzi Watendaji wa Marekani wenye asili ya China, Bw Robert Sun.

Dk Mathuki alimkaribisha Bw Sun mjini Arusha Jumanne ili kujadiliana kuhusu fursa za uwekezaji katika nchi zote washirika wa EAC.

Viongozi hao wawili walijadili mipango ya EAC kuandaa Mkutano huo unaotarajiwa kuvutia zaidi ya Wakurugenzi na wawekezaji 500 kutoka China na Marekani, ambao wanatafuta fursa za uwekezaji katika EAC.