Deni la Kenya laongezeka kwa asilimia 18%
2023-08-17 09:13:54| cri

Kenya imekopa kiwango cha juu zaidi cha pesa katika kipindi cha mwaka mmoja na kupitisha kiwango cha deni ambacho nchini inafaa kukopa kwa mjibu wa katiba. Kwa mjibu wa benki kuu ya Kenya viwango vya ukusanyaji  ushuru bado kipo chini hali ambayo imeilazimu serikali kukopa zaidi kufadhili oparesheni zake za ndani. 

Deni la taifa lilipanda kwa asilimia 18%, na kupita dola bilioni 69.52 ambazo Kenya inafaa kukopa kwa mjibu wa katiba. Hata hivyo mwezi Juni bunge la Kenya lilipitisha mwaswada unaoruhusu serikali kukopa angalau asilimia 55% ya pato la taifa kikiwa ni kiwango cha juu zaidi cha deni ikilinganishwa na ilivyokuwa awali. 

Takwimu kutoka wizara ya fedha zinasema kuwa takriban dola bilioni $9.94 sawa na asilimia 91.52, ya deni jipya la taifa ni pesa ambazo zilikopwa katika miezi tisa ya kwanza ya utawala wa sasa. Kiwango kikubwa cha pesa hizo zimekopwa kutoka kwa wakopeshaji wenye kutoa mikopo nafuu kama benki ya dunia na benki ya maendeleo ya Afrika AfDB tofauti na hapo awali ambapo Kenya ilitafuta mikopo yenye riba ya juu kama Eurobond.