Mapato ya Utalii Kenya yaongezeka kwa asilimia 32%
2023-08-17 23:14:19| cri

Mapato ya Kenya kutokana na utalii yaliongezeka na kufikia shililingi bilioni 116.2 sawa na dola za Kimarekani milioni 807 katika kipindi cha miezi sita ya kwanza ya mwaka wa 2023 kufuatia kuongezeka kwa idadi ya watalii waliowasili nchini.  Ripoti ya bodi ya utalii ya Kenya KTB imesema ongezeko hilo la mapato ni la asilimia 32% ikilinganishwa na kipindi sawa mwaka wa 2022.

Idadi ya watalii waliowasili kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa Moi mjini Mombasa, Uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta iliongezeka kutoka watalii 642, 861 hadi 847, 810 katika miezi sita ya kwanza ya mwaka huu. Kati ya watalii 847,810 waliowasili Kenya wengi walitoka Marekani (118,480), ikifuatiwa na Uganda (89,968), Tanzania (69,777), Uingereza (65,563), na India (42,805).