Je, moto wa msituni kisiwani Maui unaweza kuwaamsha wanasiasa wa Marekani au la?
2023-08-17 22:29:29| CRI

Hadi kufikia tarehe 17, moto uliotokea kwenye Kisiwa cha Maui, Hawaii, Marekani umesababisha vifo vya watu zaidi ya mia moja, na wengine zaidi ya elfu moja kutojulikana walipo, huku maelfu ya nyumba zikiteketea, ambapo hadi sasa bado haujadhibitiwa kabisa. Wamarekani wametoa shutuma kwa hasira kubwa mbele ya kamera za vyombo vya habari na kwenye mtandao wa kijamii.

Hii ni ajali mbaya zaidi ya moto wa msituni kutokea nchini Marekani katika zaidi ya miaka mia moja iliyopita. Je, chanzo chake ni nini? Baada ya mambo halisi mengi zaidi kufichuliwa, watu wamegundua kuwa kama ajali nyingi zilizotokea nchini Marekani hapo awali, ajali hiyo si kama tu ni janga la asili, bali pia ni la kibinadamu.

Ikiwa nchi yenye nguvu zaidi duniani, Marekani haina upungufu wa fedha wala teknolojia, lakini uwezo wake wa kukabiliana na maafa siku zote unakosolewa na watu. Kuanzia kubomoka kwa jengo jimboni Florida mwaka 2021, hadi ajali ya kutodhibitiwa kwa treni jimboni Ohio ya mwaka 2023, na ajali ya moto unaosambaa kisiwani Maui, Wamarekani kwa mara nyingine tena wamekata tamaa kwa uokoaji wa nchi yao.

Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya Marekani, Hawaii ina mfumo kamili wa tahadhari za usalama wa umma, ambao una kengele 400 na 80 kati yao zimefungwa kwenye Kisiwa cha Maui. Hata hivyo, kengele hizo hazikufanya kazi wakati moto ulipotokea kisiwani Maui. Watu walikosoa kuwa serikali haikukata umeme kwa wakati na hivyo kuzidisha makali ya moto. Aidha mmiliki wa mgahawa wa eneo hilo aliandika kwenye mtandao wa kijamii kuwa, Kisiwa cha Maui kiko umbali wa maili 100 tu kutoka kituo cha jeshi la eneo hilo. Hata hivyo saa 72 baada ya kutokea kwa maafa hayo, Jeshi la wanamaji la Marekani, meli za huduma za tiba, helikopta, Jeshi la nchi kavu na vifaa vya uokoaji vilifikia katika eneo la maafa. Gazeti la Washington Post limesema kuwa shughuli za uokoaji zenye ufanisi ziliandaliwa na wakazi wa huko badala ya serikali ya Marekani.

Hayo yote yameonesha upuuzi wa wanasiasa wa Marekani kwa wananchi.

Moto wa msituni ni ajali ya kawaida huko Hawaii. Mwaka 2022 Hawaii ilitangaza ripoti kuhusu majanga mbalimbali ya asili yatakayoweza kusababisha madhara mabaya, yakiwa ni pamoja na tsunami, matetemeko ya ardhi, milipuko ya volkeno, na moto wa msituni. Lakini kiwango cha hatari ya moto wa msituni kilitathminiwa kuwa ni cha “chini”, hali ambayo ilikosolewa na vyombo vya habari kama ni mwamko dhaifu wa kukabiliana na maafa.

Jambo la kusikitisha ni kuwa, wakati jeshi la Marekani lilipoondoka huko Kabul mwaka 2021, na wakati Kisiwa cha Maui kilipokumbwa na moto wa msituni mwaka 2023, rais Joe Biden alikuwa likizo, na hata wakati alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu hali ya vifo na majeruhi kisiwani Maui alijibu kwa tabasamu kuwa “hawezi kutoa maelezo yoyote”. Wanamtandao wengi walitoa shutuma kuwa rais wa Marekani angewezaje kucheka mbele ya idadi kubwa ya vifo na majeruhi ya watu. Shirika la habari la Ufaransa AFP limeeleza kuwa, moto huo mkubwa umeamsha hasira za watu kwa serikali.

Moto wa msituni unaoendelea kuwaka kisiwani Maui si kama tu umeteketeza nyumba za Wamarekani wengi, bali pia umeonesha upuuzi wa wanasiasa na upungufu wa mfumo wa Marekani. Mbele ya ukosoaji mkali wa wananchi na jumuiya ya kimataifa, je, wanasiasa wa Marekani waliotoka likizo wataweza kuzinduka au la, na kuzingatia kuzima moto nchini ili kuwaokoa wananchi wake wenye uchungu badala ya kuendeleza vitendo vya kuchochea migogoro duniani?