Sudan Kusini kuongeza bajeti yake kwa asilimia 33%
2023-08-17 09:13:28| cri

Sudan Kusini inalenga kuongeza bajeti yake ya kitaifa kwa asilimia 33% licha ya Marekani kutoa onyo kwa taifa hilo ikisema inatumia vibaya pesa za umma. Jumatatu rais Salva Kiir alitia sanini mswada wa fedha ambao ulipitishwa na bunge unaoruhusu serikali kuongeza bajeti yake wa asilimia 33%. 

Mabadiliko hayo ambayo waziri wa fedha amesema yatalisaidia taifa hilo changa barani Afrika kujikwamua kiuchumi yatahusisha pia kuongeza mishahara ya wafanyikazi wa umma kwa hadi asilimia 400%. kwa jumla bajeti hiyo itagharimu dola bilioni 16.2 za Kimarekani.  

Sudan Kusini inatarajia kufadhili bajeti hiyo kutokana na mauzo ya mafuta. Hata hivyo vita katika nchi jirani ya Sudan ambayo Sudan Kusini huiuzia mafuta huenda vikalemaza mpango huo. Ikumbukwe kuwa zaidi ya asilimia 90% ya pato la kitafa la Sudan Kusini yanatokana na mauzo ya mafuta japo pesa hizo zinafujwa sana na utawala wa awali na utawala wa sasa.