Mkuu wa Kituo cha Operesheni za Dharura cha Jamhuri ya Dominika Bw. Mendes amesema mlipuko uliotokea tarehe 14 huko San Cristobal, magharibi mwa mji mkuu wa nchi hiyo Santo Domingo umesababisha vifo vya watu 27.
Bw. Mendes amesema kwenye mkutano na wanahabari siku hiyo kwamba waokoaji wamepata miili yote ya watu waliopotea, lakini bado itachukua muda kuthibitisha utambulisho wao. Amesema mlipuko huo uliharibu maduka 13, ambapo maduka manne yameteketezwa.
Ikuli ya Jamhuri ya Dominika ilitangaza tarehe 17 mwezi huu kuwa siku ya kitaifa ya maombolezo, na bendera ya taifa itapeperushwa nusu mlingoti katika vituo vya kijeshi na majengo ya umma kote nchini.