Msukosuko katika soko la kimataifa ukaathiri usambazaji wa nafaka hasa ngano katika nchi za Afrika mashariki
2023-08-17 09:14:59| cri

Shirika la mpango wa Chakula duniani, WFP limeonya kuwa huenda msukosuko katika soko la kimataifa ukaathiri usambazaji wa nafaka hasa ngano katika nchi za Afrika mashariki. Katika ripoti yake, WFP imesema kisitishwa kwa shughuli za kusafirisha nafaka kati ya Ukraine, Urusi na  Uturuki maarufu kama usafiri kwenye bahari ya nyeusi unaziweka nchi za Afrika mashariki kama vile Somalia, Djibuti na Sudan katika hali ngumu ya kupata bidhaa hiyo muhimu ambayo inategemewa na mamilioni ya raia.

WFP imeongeza kusema uzalishaji wa ndani wa ngano katika nchi za Afrika Mashariki ni wa chini ikilinganishwa na mahitaji ya ngano.

Kwa mjibu wa WFP, mahitaji ya ngano nchini Djibuti ni asilimia 67 huku mahitajiya zao hilo nchini Somalia yakiwa asilimia 38%. Nchini Ethipia na Kenya, mahitaji ya ngano ni asilimia 24% ya jumla ya ngano inayoagizwa kutoka nje. Djibouti na Somalia zinategemea uagizaji pekee ili kukidhi mahitaji yao ya ndani ya ngano. Huku Ethiopia ikiwa nchi ya pekee katika ukanda wa Afrika mashariki ambayo uzalishaji wake wa ndani wa ngano karibu unakidhi mahitaji yake ya ndani.

Tangu Julai 2022, karibu tani 876,000 za chakula zilisafirishwa kwenda Djibouti, Ethiopia, Kenya, Somalia na Sudan kutokana na Mpango wa Nafaka wa Bahari Nyeusi, ambapo zaidi ya tani 343,000 za ngano zilisafirishwa.