Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Dk Benson Bana amesema mawasiliano na watu waliomteka nyara Mtanzania, Melkiori Mahinini nchini humo bado yanaendelea kufanyika na kwamba kijana huyo yuko salama.
Melkiori (27) ni mseminari aliyepelekwa nchini Nigeria na Shirika la Wamisionari wa Afrika, ni mzaliwa wa Kigoma katika Parokia ya Kabanga. Alikamatwa Agosti 3, 2023 katika jimbo la Minna huko Nigeria akiwa na mwenzake, Padre Paul Sanogo ambaye ni raia wa Burkina Faso.
Watekaji wanataka Naira milioni 100 (sawa na Shilingi milioni 325.1 za Tanzania) kwa ajili ya kuwaachia huru wote wawili. Kwa mtu mmoja, watekaji wanahitajika Dola za Marekani 70,000 (zaidi ya Shilingi milioni 170 za Tanzania).