Mtaalam wa Kenya asema China ni nyenzo inayoendesha mfumo wa BRICS
2023-08-17 07:50:48| CRI

Mkutano wa 15 wa viongozi wa nchi za BRICS utafanyika kuanzia tarehe 22 hadi 24 Agosti huko Johannesburg, Afrika Kusini. Akizungumzia mkutano huo, mkurugenzi mtendaji wa upande wa Kenya wa Mazungumzo kati ya Kusini na Kusini Bw. Stephen Ndegwa, amesema mkutano huo utakuwa na ajenda nyingi muhimu, na unatarajiwa kuzisaidia nchi zinazoendelea kutatua masuala halisi.

Bw. Ndegwa amesema ajenda kuu ya mkutano huo ni upanuzi wa mfumo wa BRICS, kwa kuwa nchi nyingi zinatarajia kujiunga na mfumo huo, hali inayoonesha kuwa nchi zinazoendelea duniani zinajifunza uzoefu wa mafanikio.

Ameongeza kuwa mkutano huo huenda pia utajadili sera ya sarafu, kwa lengo la kupunguza utegemezi kwa dola ya kimarekani.

Bw. Ndegwa amesisitiza kuwa China ikiwa ni nchi kubwa zaidi inayoendelea duniani, imekuwa nyenzo ya kuendesha mfumo wa BRICS, na mafanikio yake yanaonesha kuwa nchi zinazoendelea zinaweza kuondokana na umaskini.