Afrika inaweza kuwa mshiriki katika minyororo ya ugavi duniani kwa kutumia madini
2023-08-17 07:59:42| CRI

Ripoti iliyotolewa na Shirika la Biashara na Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNCTAD) inasema Afrika inaweza kuwa mshiriki mkuu katika minyororo ya ugavi duniani kwa kutumia raslimali zake za madini zinazohitajika kwenye sekta ya teknolojia ya juu.

Kwenye ripoti yake iliyotolewa mjini Nairobi, UNCTAD imesema Afrika ina hazina kubwa ya madini na metali muhimu, ikiwa ni pamoja na alumini, kobalti, shaba, lithiamu na manganisi ambayo ni muhimu kwa minyororo ya ugavi duniani.

Ripoti hiyo imetolewa wakati minyororo ya ugavi duniani imekumbwa na shinikizo kubwa kutokana na mtikisiko wa biashara duniani, sintofahamu ya kiuchumi, matukio ya kijiografia na majanga ya asili.

Ripoti imesema Afrika yenye maliasili nyingi zinazohitajika katika sekta ya nishati, magari na elektroniki, inaweza kuwa na fursa kwenye minyororo ya ugavi wa kimataifa.