Rais wa Kenya atoa wito wa mageuzi katika masuala ya fedha duniani ili kuchochea uwekezaji
2023-08-18 08:34:47| CRI

Rais William Ruto wa Kenya ametoa wito wa kufanyika kwa mageuzi katika mfumo wa fedha wa kimataifa ili kusaidia kuongeza imani ya wawekezaji barani Afrika.

Akiongea mjini Nairobi kwenye mkutano wa Shirika la maendeleo na biashara la Umoja wa Mataifa (UNCTAD), Rais Ruto amesema kuondoa hatari ya kifedha kwa nchi za Afrika kutahimiza uhusiano bora kati ya sekta ya umma na sekta binafsi kwa manufaa ya wote.

Rais Ruto amesema ni vigumu kwa sekta binafsi barani Afrika kupata pesa, kama suala la hatari za kifedha halitatatuliwa. Rais Ruto ameongeza kuwa mfumo wa sasa wa kifedha unataja kimakosa eneo la kusini mwa dunia kama eneo lenye hatari ya uwekezaji, na kuleta matokeo mabaya kwa bara la Afrika.