Watu sita wauawa katika mapigano kati ya koo kaskazini mashariki mwa Kenya
2023-08-18 08:55:59| CRI

Watu wasiopungua sita wameuawa kwa kupigwa risasi kwenye mapigano baina ya koo yaliyotokea katika kijiji kimoja cha kaunti ya Garissa nchini Kenya.

Kamishna wa eneo la Kaskazini Mashariki Bw. John Otieno amesema waliouawa walikuwa wakisafiri kwa gari wakati watu wenye silaha wasiojulikana walipowafyatulia risasi na kuwaua. Shambulizi hilo linadhaniwa kuwa ni kitendo cha kulipiza kisasi baada ya mtu mwingine wa ukoo hasimu kuuawa, mshukiwa mmoja amekamatwa na sasa anasaidia uchunguzi.

Bw. Otieno ameongeza kuwa watu wasiopungua 10 kutoka kila moja ya koo hizo wameuawa katika mapigano yanayosemekana kusababishwa na mgogoro wa muda mrefu wa ardhi.