Naibu rais wa Kenya akutana na mkuu wa shirika la habari la Xinhua
2023-08-18 08:46:34| CRI

Naibu rais wa Kenya Bw. Rigathi Gachagua amekutana na rais wa Shirika la Habari la Xinhua la China Fu Hua, na kukubaliana kuimarisha ushirikiano wa vyombo vya habari.

Bw. Gachagua amesema huu ni mwaka wa maadhimisho ya miaka 60 ya uhusiano wa kibalozi kati ya Kenya na China, na nchi hizo mbili zimehimiza imara ushirikiano wenye ufanisi na kufurahia mawasiliano ya karibu ya watu.

Bwana Gachagua amesema Kenya inapenda kuwa na uhusiano wa kiwenzi na Xinhua katika kuimarisha ushirikiano kwenye maeneo ya ripoti ya data, kutumia teknolojia ikiwemo akili bandia na uvumbuzi mwingine kwenye habari.

Bw. Fu amesema Xinhua ikiwa shirika la habari la taifa la China lenye ushawishi mkubwa duniani, imekuwa na historia ndefu ya kujulisha China kwa Afrika na kuripoti habari za Afrika kwa dunia, ikichangia kuimarishwa kwa maelewano ya pande mbili na mawasiliano ya watu kati ya China na Afrika.