Rais Xi Jinping wa China kuhudhuria mkutano wa 15 wa kilele wa BRICS na kufanya ziara Afrika Kusini
2023-08-18 10:34:33| cri

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bi Hua Chunying amesema, kutokana na mwaliko wa rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, rais Xi Jinping wa China Agosti 21 hadi 24 atahudhuria mkutano wa 15 wa viongozi wa nchi za BRICS utakaofanyika huko Johannesburg na kufanya ziara ya kitaifa nchini Afrika Kusini.

Katika ziara yake, rais Xi na mwenzake Ramaphosa wataongoza kwa pamoja mazungumzo kati ya viongozi wa China na Afrika.