Afrika Kusini yaahidi kuandaa mkutano wa kilele wa BRICS katika mazingira salama
2023-08-18 09:02:47| CRI

Shirika la taifa la utekelezaji wa sheria la Afrika Kusini limesema "vurugu na uhalifu”havitatokea wakati wa mkutano wa 15 wa kilele wa BRICS unaotarajiwa kufanyika huko Johannesburg kuanzia tarehe 22 hadi 24 mwezi huu.

Naibu Kamishina wa Polisi ya Taifa Bibi Tebello Mosikili, amesema maandalizi ya ulinzi na usalama kwa ajili ya mkutano huo yanaendelea vizuri, huku wahusika wote muhimu wakiwa tayari kutekeleza majukumu yao kulingana na mamlaka waliyopewa. Pia amesema Afrika Kusini iko tayari kuwapokea viongozi wa BRICS katika mazingira salama.