Wanajeshi 36 wauawa katikati ya Nigeria
2023-08-18 13:57:52| cri

Jeshi la Nigeria limesema wanajeshi 36 wameuawa Jumatatu katika shambulio la ghafla lililofanywa na magaidi, kwenye jimbo la Niger katikati ya nchi hiyo.

Msemaji wa jeshi hilo Edward Buba amewaambia wanahabari mjini Abuja, mji mkuu wa Nigeria, kuwa shambulio hilo lilifanywa na magaidi wa kundi lisilojulikani Jumatatu karibu kijiji cha Zungeru katika jimbo la Niger. Ameongeza kuwa, helikopta moja ya jeshi iliyotumiwa kusafirisha majeruhi ilikutwa imeanguka karibu na eneo la tukio, na kuongeza idadi ya vifo.

Alisema uchunguzi unaendelea kugundua chanzo cha kuanguka kwa helikopta hiyo.

Mashambulizi mfululizo yanayofanywa na watu wenye silaha yametokea hivi karibuni nchini Nigeria, na kusababisha vifo vya raia na maofisa usalama nchini humo.