China yatoa Dola Milioni moja kwa UM kuwasaidia watoto wakimbizi wa Palestina
2023-08-18 08:35:30| CRI

China imetoa dola milioni 1 za Kimarekani ili kusaidia mpango wa elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Palestina (UNRWA).

Mkuu wa Ofisi ya China kwa taifa la Palestina Bw. Zeng Jixin, alitia saini makubaliano ya kutoa msaada huo na Bw. Karim Amer, mkurugenzi wa Ushirikiano wa UNRWA. Msaada huo utawanufaisha watoto wakimbizi 5,300 katika shule tano za shirika hilo kwenye ukanda wa Gaza.

Bw. Zeng amesema China inatambua na kupongeza kazi ya UNRWA na imekuwa ikitoa msaada kwa shirika hilo kadiri inavyoweza ili kulisaidia kutekeleza majukumu yake, na kuongeza kuwa China iko tayari kufanya kazi na jumuiya ya kimataifa ili kutoa mchango chanya kuelekea suluhu la kudumu ya suala la Palestina.