Uongozi wa CPC wapanga kazi kuhusu uzuiaji wa mafurikio na ujenzi baada ya maafa
2023-08-18 08:22:56| CRI

Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) imekutana jana Agosti 17 kutafiti na kupanga kazi kuhusu uzuiaji na uokoaji wakati wa mafuriko na ujenzi upya wa maeneo yaliyoathiriwa na maafa.

Katibu mkuu wa Kamati Kuu ya CPC Bw. Xi Jinping, ameongoza mkutano huo na kutoa hotuba muhimu.

Mkutano huo umesema, China imepata maendeleo makubwa kwenye kazi ya kuzuia mafuriko na uokoaji baada ya maafa, lakini juhudi za bila kusita zinatakiwa kufanywa wakati hatari za kutokea mafuriko kwenye mito kadhaa bado zipo na hatari za kutokea mafuriko milimani kwenye baadhi ya maeneo ya kaskazini na kaskazini mashariki mwa China bado ziko juu. Wakati huohuo, ukame ambao umetokea katika maeneo kadhaa haupaswi kupuuzwa.

Kamati hiyo imezitaka serikali za mitaa na idara husika kuweka kipaumbele kwa usalama wa maisha ya watu na mali zao, na kuendelea kufanya kazi nzuri kwenye uzuiaji wa mafuriko na uokoaji baada ya maafa.