Kwa nini eneo la Afrika Mashariki liko katika hatari ya magonjwa ya wanyama yanayosambazwa kwa binadamu
2023-08-19 12:16:03| cri

Wataalamu wameonya kuwa kanda ya Afrika Mashariki iko katika hatari ya magonjwa yanayoambukiza kutoka kwa wanayama, ikiwa ni pamoja na yale kutoka kwa wanyama pori. Hii ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Traffic, Shirika yasiyo ya kiserikali ya kimataifa ambayo inajulikana kama mtandao wa ufuatiliaji wa biashara ya wanyamapori.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa magonjwa haya yanawezekana kuchochewa na ongezeko la joto ambalo linafaa kwa uenezaji wa vimelea vya magonjwa. Kutokana na mifugo na wanyamapori wengi kutembea kwa uhuru na miingiliano yao na wanadamu, hatari za maambukizi zinaweza kuwa kubwa zaidi. Hali ya hewa ya kitropiki ya Afrika Mashariki inafaa kwa hatari za maambukizi ya magonjwa mbalimbali kutoka kwa wanyama hadi binadamu. Dk Daniel Mdetele, mtaalam wa mifugo, anasema maambukizi haya hayasababishi magonjwa na vifo tu bali huvuruga biashara.