AU yatoa wito wa kukomesha mara moja uhasama nchini Libya
2023-08-19 22:14:45| cri

Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AU) Bw. Moussa Faki Mahamat Alhamisi alitoa wito wa kukomesha mara moja uhasama nchini Libya.

Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, Bw. Faki alihimiza wadau wote husika ikiwa ni pamoja na wa kijeshi, kisiasa na kijamii nchini Libya wamalize mara moja uhasama.

Mapigano kati ya wanamgambo wa kikosi kiitwacho 444 na mahasimu wao wa Kikosi Maalumu yalitokea usiku wa Jumatatu katika baadhi ya sehemu za Tripoli baada ya kuripotiwa kuwa kikosi hicho kimemkamata kamanda wa kikosi cha 444.

Hadi sasa, watu 55 waliuawa na wengine 126 kujeruhiwa katika mapigano yaliyolipuka kwenye mji mkuu wa Libya.