Naibu spika wa Bunge la Afrika Kusini akutana na mkuu wa Shirika Kuu la Utangazaji la China
2023-08-20 15:14:19| CRI

Naibu spika wa Bunge la Afrika Kusini Bw. Solomon Lechesa Tsenoli jana alikutana na mkuu wa Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) Bw. Shen Haixiong ambaye yuko ziarani mjini Cape Town, ambapo Bw. Tsenoli alipongeza kufikiwa kwa makubaliano ya ushirikiano kati ya CMG na kampuni ya MultiChoice ambayo ina jukwaa kubwa zaidi la satelaiti la utangazaji wa moja kwa moja barani Afrika.

Kwa mujibu wa makubaliano hayo,shirika la CMG litatoa idhini kwa kampuni ya MultiChoice kutangaza vipindi vyake vya chaneli ya CCTV-4 , chaneli ya Kiingereza na chaneli ya Kifaransa ya CGTN barani Afrika, ambazo zinatoa huduma katika zaidi ya nchi 50 za Afrika.

Bw. Tsenoli alisema kuwa pande mbalimbali za jamii ya Afrika Kusini zinatarajia kwa hamu kubwa ziara ya Rais Xi Jinping wa China nchini humo na anaamini kwamba nchi hizo mbili zenye urafiki wa kindugu zitapata mafanikio zaidi kwenya ushirikiano katika nyanja mbalimbali na kuhimiza utaratibu wa kimataifa uendelezwe kwa mwelekeo wa haki na halali.

Kwa upande wake, Bw.Shen alisema kuwa mwaka huu ni kumbukumbu ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Afrika Kusini na maadhimisho ya miaka 10 ya pendekezo la "Ukanda Mmoja,Njia Moja”. Chini ya uongozi wa wakuu wa nchi hizo mbili, mawasiliano na ushirikiano kati ya pande hizi yamehimizwa zaidi. CMG linapenda kuimarisha ushirikiano na Bunge la Afrika Kusini na kuchangia ujenzi wa jumuiya yenye hatma ya pamoja ya kiwango cha juu kati ya China na Afrika Kusini.