CMG yasaini makubaliano ya ushirikiano na vyombo vya habari vya Afrika
2023-08-21 14:22:09| CRI

Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) limesaini makubaliano ya ushirikiano na vyombo vya habari vya nchi za Afrika ikiwemo Umoja wa Utangazaji wa Afrika na Shirika la Utangazaji la Afrika Kusini jana Jumapili huko Johannesburg, Afrika Kusini.

Makubaliano hayo yamesainiwa wakati rais wa China Xi Jinping anaposhiriki katika Mkutano wa 15 wa viongozi wa BRICS na kufanya ziara ya kiserikali nchini Afrika Kusini.

Katika ujumbe wake, Naibu mwenyekiti wa Chama cha ANC cha Afrika Kusini ambaye pia ni makamu wa rais wa nchi hiyo, Paul Mashatile ameutakia ushirikiano kati ya CMG na wenzi wake wa vyombo vya habari wa Afrika kupata mafanikio mazuri. Pia ameeleza kuwa juhudi zinazofanywa na CMG katika kukuza ushirikiano wa vyombo vya habari kati ya Afrika na China zinatia moyo sana, na anatarajia pande hizo mbili zitahimiza mawasiliano ya utamaduni na faida za kunufaishana kupitia ushirikiano wa vyombo vya habari.