Sehemu ya pili ya Nukuu bora za Xi Jinping yazinduliwa barani Afrika
2023-08-21 09:18:45| CRI

Uzinduzi wa matoleo ya Kiingereza, Kifaransa, Kiarabu, Kihausa na Kiswahili ya Sehemu ya pili ya Nukuu bora za Xi Jinping umefanyika tarehe 20, Agosti, mjini Johannesburg, Afrika Kusini. Kipindi cha Nukuu bora za Xi Jinping kimeanza kuoneshwa kuanzia siku hiyo hiyo katika vyombo vikuu vya habari vya nchi 38 za Afrika.

Makamu wa rais wa Afrika Kusini Paul Mashatile na naibu spika wa bunge la Afrika Kusini Lechesa Tsenoli wametoa pongezi kwa uzinduzi wa kipindi hiki, wakisema kurushwa kwa kipindi hiki ni muhimu kwa nchi mbalimbali za Afrika kufahamu busara ya rais Xi Jinping kuhusu utawala wa nchi na kujua chanzo cha mabadiliko ya China katika zama mpya.

Mkuu wa kituo kikuu cha radio na televisheni cha China Bw. Shen Haixiong, balozi wa China nchini Afrika Kusini Bw. Chen Xiaodong na wageni wengine wamehudhuria uzinduzi huo.