China yafanikiwa kurusha setilaiti mpya ya uchunguzi wa sayari ya dunia
2023-08-21 09:16:45| CRI

China imerusha setilaiti mpya ya uchunguzi wa sayari ya dunia leo Jumatatu kwenye kituo cha kurushia setilaiti cha Jiuquan, kaskazini magharibi mwa China.

Setilaiti hiyo iitwayo Gaofen-12 04 imerushwa kwa roketi ya Changzheng-4C na kufanikiwa kuingia kwenye njia yake ya obiti. Setilaiti hiyo itafanya kazi kwenye nyanja mbalimbali, zikiwa ni pamoja na uchunguzi wa ardhi, mipango miji, usanifu wa mtandao wa barabara, makadirio ya uzalishaji wa mazao na uokoaji wa maafa.