Majadiliano ya kuiruhusu Somalia kuwa mwanachama wa EAC kuanza kesho
2023-08-21 14:29:57| cri

Majadiliano kati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Somalia kuhusu nchi hiyo kuwa mwanachama wa EAC yanatarajiwa kuanza kesho jumanne mjini Nairobi, Kenya.

Mwezi Februari mwaka huu, mkutano wa 43 wa kawaida wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulifanyika nchini Burundi kutathmini ripoti ya kuridhia Somalia kuwa nchi mwanachama wa Jumuiya hiyo.

Taarifa iliyotolewa na Makao Makuu ya Jumuiya hiyo mjini Arusha, Tanzania, imesema, jukumu la uhakiki limekamilisha ripoti yake baada ya kufanya ziara nchini Somalia kuanzia Januari 25 hadi Februari 5 mwaka huu.

Endapo Somalia itajiunga na Jumuiya hiyo, itaongeza idadi ya nchi wanachama kuwa nane. Hivi sasa nchi wanachama wa EAC ni Burundi, Kenya, Tanzania, Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Rwanda, na Sudan Kusini.