Ushirikiano kati ya CMG na Kundi la MultiChoice wapongezwa nchini Afrika Kusini
2023-08-21 14:32:25| cri

Naibu Spika wa Bunge la Afrika Kusini Solomon Lechasa Tsenoli amekutana na Rais wa Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) Shen Haixiong mjini Cape Town, na kupongeza makubaliano ya ushirikiano yaliyofikiwa kati ya CMG na Kundi la MultiChoice la Afrika Kusini.

Bw. Lechasa amesema Afrika Kusini na China, ambao ni ndugu wa karibu, wanavuna kwa pamoja manufaa ya ushirikiano wa kina, na kuwa nguvu ya kuongoza utaratibu wa kimataifa kuwa wa haki na usawa.

Kwa upande wake, Bw. Shen amesema mwaka huu ni miaka 25 tangu kuanza kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili, na ni maadhimisho ya miaka 10 tangu China ilipotoa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja. Amesema CMG inapenda kuimarisha ushirikiano na Bunge la Afrika Kusini na kutoa mchango katika kujenga jamii ya ngazi ya juu ya China na Afrika Kusini yenye mustakabali wa pamoja.