Sehemu ya pili ya filamu maalum ya ‘Nukuu za Fasihi Anazopenda Xi Jinping’ yatangazwa barani Afrika
2023-08-21 11:22:05| CRI

Wakati Rais Xi Jinping wa China anahudhuria Mkutano wa 15 wa kilele wa nchi za BRICS na kufanya ziara ya kitaifa nchini Afrika Kusini, sehemu ya pili ya filamu maalumu ya 'Nukuu za Fasihi Anazopenda Xi Jinping’kwa lugha mbalimbali zikiwemo Kiingereza, Kifaransa, Kiarabu, Kihausa na Kiswahili, limezinduliwa rasmi jana Agosti 20 huko Johannesburg, na linatarajiwa kuoneshwa kupitia vyombo vikuu vya habari 62 katika nchi 38 za Afrika.

Sehemu ya pili ya‘Nukuu za Fasihi Anazopenda Xi Jinping’ imechagua kwa makini nukuu za fasihi alizowahi kutumia Rais Xi Jinping kwenye hotuba, makala na kauli zake, ambazo zimeonesha hazina yake kubwa ya utamaduni na moyo wake wa dhati wa kujali mustakbali wa taifa na kutoa kipaumbele maslahi ya wananchi, na pia zimefafanua alama maalumu za kiroho za ustaarabu wa China, undani wake katika zama mpya na thamani yake kwa utandawazi.

Naibu mwenyekiti wa Chama cha ANC cha Afrika Kusini na makamu wa rais wa nchi hiyo, Paul Mashatile ametoa taarifa ya pongezi kwa Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG kuzindua sehemu ya pili ya filamu hiyo maalumu barani Afrika. Bw. Mashatile amesema, uhusiano wa kibalozi kati ya China na Afrika Kusini umetimiza miaka 25, na Afrika Kusini inapenda kuendeleza urafiki mkubwa kati ya pande hizo mbili. Afrika na China zinaweza kusukuma mbele utawala wa nchi na maendeleo ya jamii kupitia nguvu ya vyombo vya habari.

Akihutubia sherehe ya uzinduzi wa filamu hiyo, Naibu Mkuu wa Idara ya Uenezi ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mkuu wa Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) Bw. Shen Haixiong amesema, huu ni mwaka wa kumi tangu Rais Xi Jinping wa China alipotoa mwongozo wa kuzingatia udhati, uhalisi, undugu na uaminifu kwenye sera ya China kwa Afrika na mtazamo sahihi kuhusu haki na maslahi kwenye ushirikiano kati ya China na Afrika. Anaamini kuwa sehemu ya pili ya filamu hiyo itafungua dirisha kwa marafiki wa Afrika kuelewa fikra za Rais Xi Jinping kuhusu utawala wa nchi, kufahamu vizuri zaidi utamaduni wa China, busara za China na moyo wa China, kujisikia kwa kina mvuto maalumu wa ujenzi wa ustaarabu wa kisasa wa taifa la China, na kujionea China inayoaminika, inayopendeza na inayoheshimika katika zama mpya.