Wajumbe ECOWAS wakutana na Rais wa Niger aliyepinduliwa
2023-08-21 23:28:37| cri

Ujumbe kutoka Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) umekutana na Rais Mohamed Bazoum wa Niger ambaye alipinduliwa mwezi Julai mwaka huu.

Ujumbe huo unaoongozwa na Rais wa zamani wa Nigeria, Abdulsalami Abubakar, umekutana na Rais Bazoum ikiwa ni siku moja baada ya mkutano wa wakuu wa majeshi wa nchi wanachama wa ECOWAS uliofanyika mjini Accra, Ghana. Mkutano huo ulifanyika mbele ya Waziri Mkuu aliyeteuliwa na viongozi wa mapinduzi, Mahamane Lamine Zeine na mjumbe mwingine wa utawala wa kijeshi, lakini hakuna taarifa zilizotolewa kuhusu mazungumzo yao.

Awali, viongozi hao walikutana na wajumbe wa serikali ya kijeshi, akiwemo Jenerali Abdurahmane Tiani na walitaka kurejeshwa kwa utawala wa kikatiba nchini Niger.