Usafirishaji wa ng'ombe nchini Sudan waendelea licha ya mapigano
2023-08-21 09:18:03| CRI

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Rasilimali za Wanyama na Uvuvi wa Sudan Bw. Hasan Mugrari amesema katika taarifa kwamba hadi sasa nchi hiyo imeuza nje ng'ombe milioni 2.7 mwaka huu.

Ameongeza kuwa usafirishaji wa mifugo kwenda Saudi Arabia na nchi nyingine uliendelea licha ya hali ya vita. Ili kufidia kusimamishwa kwa mauzo ya nje kutoka jimbo la Khartoum kutokana na vita, wizara imeanzisha machinjio katika majimbo mengine ili kuuza nyama nje.

Kulingana na takwimu za Kituo cha Utafiti wa Uzalishaji Wanyama nchini humo, Sudan ina takriban ng'ombe milioni 107. Mifugo inachangia asilimia zaidi ya 25 ya mapato ya nje ya Sudan na asilimia zaidi ya 20 ya Pato la Taifa.