China yafanikiwa kurusha setilaiti mpya ya kufuatilia Dunia
2023-08-22 13:13:53| cri

China imerusha kwa mafanikio setilaiti mpya katika anga za juu kutokea kwenye Kituo cha Kurusha Setilaiti cha Jiuquan, kaskazini magharibi mwa China.

Setilaiti hiyo, Gaofen-12 04, iliyorushwa kwa kutumia roketi ya Long March 4C, imeingia kwenye mzunguko uliopangwa kwa mafanikio. Setilaiti hiyo itatumika katika maeneo mbalimbali, ikiwemo utafiti, mipango ya miji, makadirio ya mavuno, na kutoa misaada katika majanga.