Xi awasili Afrika Kusini kwenye mkutano wa 15 wa wakuu wa BRICS na ziara ya kiserikali
2023-08-22 09:11:19| CRI

Rais Xi Jinping wa China aliwasili Afrika Kusini Jumatatu ili kuhudhuria mkutano wa 15 wa wakuu wa nchi za BRICS utakaoanza leo Johannesburg, na kufanya ziara ya kiserikali nchini humo. Akiwa nchini humo, Xi ataongoza Mazungumzo ya Viongozi wa China na Afrika pamoja na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa.

Wakati huohuo katika makala yenye kichwa "Kuendesha Meli Kubwa ya Urafiki na Ushirikiano kati ya China na Afrika Kusini kuelekea kwenye Mafanikio Makubwa," iliyochapishwa Jumatatu katika vyombo vya habari vya Afrika Kusini, rais Xi alisema uhusiano unaostawi kati ya China na Afrika Kusini ni moja ya mahusiano ya nchi mbili yenye nguvu zaidi katika ulimwengu wa nchi zinaoendelea na kwamba "umeingia katika 'zama za dhahabu,' zenye matarajio mapana na mustakabali wenye matumaini."

Kwa upande wake Sifiso Mahlangu, mhariri mkuu wa gazeti maarufu la Afrika Kusini, The Star, ambalo lilichapisha makala hii na ile ya mwaka 2015 ambazo zote mbili zilisainiwa na rais Xi, alisema wakati dunia inakabiliwa na hali nyingi zenye utata na kuishi kupitia mabadiliko ya kasi ambayo hayajawahi kuonekana katika karne moja, mfano huo wa  “Meli Kubwa” bado una ukweli.