Msomi wa Cameroon: “Ukanda Moja, Njia Moja” watoa mchango katika kuboresha maisha ya watu wa Cameroon
2023-08-22 15:21:55| CRI

Huu ni mwaka wa kumi tangu pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, Mwongozo wa kuzingatia udhati, uhalisi, undugu na uaminifu kwenye sera ya China kwa Afrika na Mtazamo sahihi wa haki na maslahi kwenye ushirikiano kati ya China na Afrika vilipotolewa. Akihojiwa hivi karibuni na Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG, msomi wa Cameroon Dkt. Taling Tene Rodrigue amesema, katika muongo mmoja uliopita, pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” limetoa fursa za kutimiza malengo ya maendeleo kwa nchi zinazoendelea, zikiwemo nchi za Afrika.

 

Dkt. Rodrigue, ambaye ni naibu mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa nchi zinazotumia Kifaransa cha Taasisi ya Utafiti wa Afrika katika Chuo Kikuu cha Ualimu cha Zhejiang, amesema katika muda mrefu uliopita, dunia nzima imekuwa ikikabiliwa na pengo kubwa la fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu, pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” limehimiza uwekezaji kwenye sekta ya miundombinu, ili kuharakisha muunganiko kati ya China na Dunia na maendeleo ya pamoja. Nchi nyingi zimetambua thamani kubwa ya “Ukanda Mmoja, Njia Moja”. Hadi kufikia mwezi Januari mwaka huu, China imesaini nyaraka zaidi ya 200 za ushirikiano wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” na nchi 151 na mashirika 32 ya kimataifa kote duniani, na ushirikiano huo umehusisha karibu nchi zote za Afrika.

 

Dkt. Rodrigue amesema, baadhi ya vyombo vya habari vya magharibi vinamepaka matope “Ukanda Mmoja, Njia Moja” vikidai kuwa ni ushirikiano huo ndio umesababisha eti “mtego wa madeni” kwa nchi za Afrika, lengo lao likiwa ni kuhujumu ushirikiano kati ya China na Afrika. Amesema, vyombo vya habari vya magharibi haviwezi kuvumilia kuwepo kwa hali nzuri ya kunufaishana inayoshuhudiwa Afrika bila ushawishi au uongozi wa nchi za magharibi, kwa hivyo vinajaribu kuchafua na kupotosha mafanikio yaliyopatikana ya “Ukanda Mmoja, Njia Moja”. Dkt. Rodrigue anaona kwa upande wa Afrika, ushirikiano na Afrika ni wenye ufanisi na umezaa matunda mengi.

 

Dkt. Rodrigue amesema, chini ya mfumo wa pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, wanafunzi na vijana wengi wa Cameroon wamepata fursa za kujiendeleza kimasomo yaoau kupata mafunzo nchini China. China siku zote imekuwa inaendelea kutoa msaada wa matibabu kwa Cameroon, haswa kwenye kipindi cha janga la Uviko-19. Mbali na hayo, China pia imeisaidia Cameroon kujengae barabara na vituo vya umeme wa maji, na kuinua kidhahiri kiwango cha miundombinu nchini Cameroon. Msomi huyo anaona, ushirikiano wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” kati ya Cameroon na China umepata mafanikio halisi, na umetoa mchango chanya katika kuboresha maisha ya watu wa Cameroon.