Watu 23 wauawa katika shambulio nchini Mali
2023-08-22 23:15:06| cri

Watu wasiojulikana waliokuwa na silaha wamewaua watu 23 na kujeruhi wengine 12 katika shambulio lililofanywa katika kijiji kimoja katikati ya Mali.

Gavana wa jimbo la Bandiagara ambako shambulio hilo lilitokea, Sidi Mohamed El Bechir amesema, watu hao wasiojulikana walifanya mauaji hayo na kuchoma moto nyumba kadhaa katika kijiji cha Yarou.

Jamii za eneo la kati na kaskazini mwa Mali zimekuwa katika ghasia zilizodumu kwa muda mrefu za kutumia silaha tangu mwaka 2012, huku waasi wenye itikadi kali wakilazimishwa kuondoka madarakani katika miji ya kaskazini mwa Mali kwa msaada wa operesheni ya kijeshi iliyoongozwa na Ufaransa.