Mapigano makali kati ya Wanajeshi wa Sudan (SAF) na Wanajeshi wa Msaada wa Haraka (RSF) yaliendelea jana Jumatatu karibu na kambi ya kimkakati ya askari wa kivita katika eneo la kijeshi la Al-Shajara, kusini mwa mji mkuu Khartoum.
Katika taarifa msemaji wa SAF, Nabil Abdalla, alisema kwa siku ya pili, waasi walijaribu kuingia kwenye kambi ya askari wenye silaha, ambapo vikosi vya SAF viliwarudisha nyuma na kusababisha waasi wengi kuuawa pamoja na hasara kubwa ya vifaa.
Katika taarifa iliotolewa Jumatatu hiyohiyo na RSF, ilisema kwamba vikosi vyake vimepata ushindi mkubwa katika mapambano dhidi ya jeshi la kivita la SAF huko Khartoum, na kusababisha hasara kubwa miongoni mwa wanamgambo wa Al-Burhan na mabaki ya utawala uliokufa.
Taarifa hiyo ilibainisha kuwa RSF imedhibiti sehemu kubwa ya kambi ya askari wa jeshi, na kulazimisha vikosi vya SAF kukimbia na kujificha katika baadhi ya majengo karibu na kambi hiyo.
Kambi hiyo ya wanajeshi wa kivita imekuwa ikilengwa zaidi na RSF, ambapo ilifanya majaribio kadhaa ya kuidhibiti.