Nchi za BRICS zaripoti kuongezeka kwa kasi kwa biashara
2023-08-22 11:04:17| cri

Biashara kati ya China na nchi nyingine za BRICS imeendelea kuongezeka kwa kasi katika miezi saba ya mwanzo ya mwaka huu.

Takwimu rasmi zilizotolewa jana jumatatu na Idara Kuu ya Forodha ya China zinaonyesha kuwa, kati ya mwezi Januari hadi Julai, biashara ya uagizaji na uingizaji bidhaa kati ya China na nchi nyingine wanachama wa BRICS iliongezeka kwa asilimia 19.1 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana, na kufikia dola za kimarekani bilioni 330.62.

Kwa mujibu wa mamlaka za forodha, biashara kati ya China na nchi nyingine za BRICS ilichukua asilimia 10.1 ya biashara ya jumla ya nje ya China katika miezi saba ya mwanzo ya mwaka huu, ikiwa ni zaidi kwa asilimia 1.6 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hicho.