Wataalamu wakutana nchini Kenya kuhimiza usalama wa sekta ya usafiri wa anga ya Afrika
2023-08-22 09:16:51| CRI

Mkutano wa wataalamu wa usafiri wa anga umeanza huko Nairobi, mji mkuu wa Kenya ukilenga kujadili njia za kuhimiza usalama wa sekta ya usafiri wa anga ya Afrika.

Mkutano huo utakaofanyika kwa siku tano unahudhuriwa na wajumbe zaidi ya 300 kutoka idara za usimamizi wa usafiri wa anga za kimataifa na za Afrika pamoja na sekta binafsi kujadili njia za kupunguza ajali za anga barani humo.

Rais wa Baraza la Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga ICAO Salvatore Sciacchitano ametoa hotuba katika ufunguzi wa wiki ya nane ya usafiri wa anga wa Afrika na Bahari ya Hindi akisema, mkutano huo ni alama ya hatua kubwa ya kuelekea kuhakikisha usalama wa mashirika ya ndege barani Afrika, kwa sababu utatoa mapendekezo juu ya hatua za kupunguza uwezekano wa hatari za hewa.